MAREKANI-COVID 19

Rais Biden alenga kumaliza maambukizi ya Covid 19 ifikapo Julai 4.

Rais wa Marekani Joe Biden, akilihotubia taifa Machi 10, 2021 kutoka Ikulu ya Washington DC.
Rais wa Marekani Joe Biden, akilihotubia taifa Machi 10, 2021 kutoka Ikulu ya Washington DC. AP - Andrew Harnik

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ana matumaini kuwa nchi hiyo inaweza kuwa huru dhidi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 kufikia tarehe nne Julai, siku ya kuadhimisha sikukuu ya uhuru wa nchi hiyo, iwapo Wamarekani wataendelea kupokea chanjo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Biden amewaambia Wamarekani kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya janga hilo wakati huu watu wote wenye umri wa makomo wanapotarajiwa  kuanza kupewa chanjo kuanzia tarehe 1 mwezi Mei.

Iwapo tutashirikiana pamoja, ifikap Julai 4, kuna nafasi nzuri kwamba wewe na família yako mtasherehekea siku ya Uhuru pamoja. amesema Biden.

Aidha, Biden amesema kuwa iwapo mambo yataenda sawa, nchi hiyo hiyo itasherehekea uhuru dhidi ya maambukizi ya Corona.

 

Biden alikuwa amepanga kutoa chanjo Milioni 100 kwa watu nchin humo ndani ya siku 100 za kuwa madarakani, lakini amesema idadi hiyo itafikiwa baada ya siku 60.

Siku ya Ijumaa, alitia saini mpango wa Matrilioni ya Dola, kuwasaidia watu walioathriwa zaidi na janga hilo.

Marekani ndilo taifa lililoathiriwa zaidi na maambukizi ya Corona dunia, baada ya watu Milioni 29 kuambukizwa na wengine zaidi ya 500,000 kupoteza maisha mpaka sasa.