BRAZILI

Coronavirus: Zaidi ya vifo 3,000 vyaripotiwa kwa kipindi cha saa 24 Brazil

Idadi ya wastani ya vifo katika siku saba zilizopita nchini Brazil imeongezeka zaidi ya mara tatu tangu kuanza kwa mwaka huu, hadi 2,364, na kuifanya kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na idadi kubwa ya vifo vya kila siku.
Idadi ya wastani ya vifo katika siku saba zilizopita nchini Brazil imeongezeka zaidi ya mara tatu tangu kuanza kwa mwaka huu, hadi 2,364, na kuifanya kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na idadi kubwa ya vifo vya kila siku. AP - Andre Penner

Brazil inaingia katika mgogoro wa afya ambao hauwezi kudhibitiwa, ikivuka kizingiti cha vifo vya watu 3,000 vya kila siku kutokana na COVID-19 kwa mara ya kwanza Jumanne  wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo yenye watu milioni 212 imerekodi vifo 3,251 katika kipindi cha saa 24 zilizopita, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya, na kusababisha jumla ya vifo kufikia 298,676 tangu kugundulika kwa kesi ya kwanza mwishoni mwa mwezi Februari 2020.

Idadi ya wastani ya vifo katika siku saba zilizopita imeongezeka zaidi ya mara tatu tangu kuanza kwa mwaka huu, hadi 2,364, na kuifanya kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na idadi kubwa ya vifo vya kila siku.

Brazil ni nchi ya pili iliyorekodi vifo vingi zaidi duniani kutokana na janga la COVID-19 kwa idadi kamili baaada ya Marekani.

Bolsonaro ategemea chanjo

Kwa jumla, nchi imerekodi visa milioni 12.1, pamoja na maambukizi mapya 82,493 katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Siku ya Jumanne jioni rais Jair Bolsonaro alihakikisha kwamba nchi yake tarejelea "maisha ya kawaida" na shughuli za kawaida zitaanza siku za usoni baada ya kupata chanjo ambayo amekosoa kwa muda mrefu.

"Ninataka kuwahakikishia raia wa Brazil na kuwajulisha kuwa chanjo zimehakikishiwa. Kufikia mwisho wa mwaka tutakuwa tumefikia zaidi ya dozi milioni 500 za chanjo kwa (kuwachanja) raia wote", alisema rais Bolsonaro.

Kufikia sasa, Wabrazil milioni 11.1, sawa na 5.2% ya raia wote wa nchi hii, wamepokea angalau dozi moja ya chanjo na watu milioni 3.5 tayari wapepokea dozi mbili, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP kutoka takwimu za rasmi.

Wakati huo huo Jair Bolsonaro, ambaye anataka kuwania tena katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2022, alielezea mshikamano wake "na wale wote ambao wamepoteza wapendwa wao".