BRAZILI

Coronavirus: Brazil yapitisha kizingiti cha vifo 300,000

Brazil ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani baada ya Marekani.
Brazil ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani baada ya Marekani. EVARISTO SA / AFP

Brazil imerekodi vifo vipya 2,009 kutokana na COVID-19 kwa siku moja, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatano wiki hii na Wizara ya Afya nchini humo, na kufikidsha jumla ya vifo 300,000.

Matangazo ya kibiashara

Karibu visa 90,000 vipya vya maambukizi pia vimegunduliwa katika kipindi cha saa ishirini na nne.

Waziri mpya wa Afya, Marcelo Queiroga, aliahidi Jumatano mchana kwamba serikali itafanya kazi ili kuharakisha kampeni ya chanjo.

Wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari, alisema lengo la serikali ilikuwa kutoa dozi milioni moja za chanjo hiyo kila siku.