BRAZILI

Coronavirus: Rekodi mpya ya vifo vya siku moja yaripotiwa nchini Brazil

Muuguzi katika katika wodi ya wagonjwa wa Covid-19 katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pedro Ernesto (HUPE) huko Rio de Janiero, Julai 15, 2020.
Muuguzi katika katika wodi ya wagonjwa wa Covid-19 katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pedro Ernesto (HUPE) huko Rio de Janiero, Julai 15, 2020. Mauro PIMENTEL / AFP

Brazil imerekodi  vifo vipya 3,780  kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya, rekodi mpya ya kila siku tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya katika nchi hii ya Amerika Kusini, moja ya nchi zilizoathirika zaidi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa kiafya nchini Brazil sasa umesababisha vifo 317,646 na zaidi ya visa milioni 12.6 vya maambukizi, wakati karibu visa vipya 85,000 vya maambukizi vimeripotiwa kwa siku moja.

Jumanne wiki hii Rais Jair Bolsonaro alisaini agizo linalotoa karibu dola bilioni 1 kwa mkopo mpya ili kukabiliana na athari za mgogoro wa kiafya.

Mikopo hii itatumika hasa kuimarisha mfumo wa afya, ilisema wizara ya fedha.

Wakati huo huo, serikali ya shirikisho imeanza majadiliano na Marekani kwa ushirikiano katika mapambano dhidi ya janga hilo.