HONDURAS

Kaka wa rais wa Honduras ahukumiwa kifungo cha maisha nchini Marekani

Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandez atoa ujumbe baada ya kaka yake Juan Antonio "Tony" Hernandez kupatikana na hatia ya ulanguzi wa madawa ya kulevya nchini Marekania, huko Tegucigalpa, Honduras Oktoba 18, 2019.
Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandez atoa ujumbe baada ya kaka yake Juan Antonio "Tony" Hernandez kupatikana na hatia ya ulanguzi wa madawa ya kulevya nchini Marekania, huko Tegucigalpa, Honduras Oktoba 18, 2019. REUTERS - JORGE CABRERA

Tony Hernandez, kaka wa rais wa sasa wa Honduras na mbunge wa zamani  nchini humo, amehukumiwa na mahakama nchini Marekani kifungo cha maisha, na miaka 30 zaidi, kwa biashara ya madawa ya kulevya.

Matangazo ya kibiashara

Ametakiwa pia kulipa dola milioni 138.5, kiasi ambacho waendesha mashtaka wamesema wanachukukulia kama ni "pesa haramu" alizopata kuptia biashara ya madawa ya kulevya.

"Hii ni biashara ya madawa ya kulevya inayofadhiliwa na serikali na hii ndio aina ya tabia ambayo serikali inapaswa kukabiliana nayo, kutokana na athari iliyo nayo kwa Honduras," amesema mwendesha mashtaka Matthew Laroche.

Waendesha mashtaka wanamshutumu Tony Hernandez, 41, kwa kupokea mamilioni ya dola ya rushwa, ikiwa ni pamoja na milioni moja kutoka kwa Joaquin Guzman, anayejulikana kama "El Chapo", tajiri wa zamani wa kampuni ya Mexico ya Sinaloa.

Fedha hizi, kulingana na waendesha mashtaka wa Marekani, zilisaidia kufadhili kampeni za uchaguzi za Chama tawala na kumnufaisha kaka wa Tony Hernandez, Rais wa sasa Juan Orlando Hernandez.

Juan Orlando Hernandez amekanusha mashtaka haya. Hajashtakiwa kwa uhalifu wowote.