MAREKANI

Marekani, Japan na Korea Kusini kukutana Ijumaa kuhusu Korea Kaskazini

Mshauri wa usalama katika Ikulu ya White House Jake Sullivan.
Mshauri wa usalama katika Ikulu ya White House Jake Sullivan. SAUL LOEB AFP

Mshauri wa usalama katika Ikulu ya White House Jake Sullivan atakutana na maafisa wa Japani na Korea Kusini Ijumaa kujadili, pamoja na mambo mengine, kudumishwa kwa amani na utulivu katika rasi ya Korea, Ikulu ya White House imesema katika taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini ilirusha kile ilichokielezea kama makombora mapya muhimu katika Bahari ya Japani wiki iliyopita, ikionyesha maendeleo katika mpango wake wa urutubishaji na kuongeza shinikizo kwa Marekani, ambapo utawala wa Biden unatathmini sera ya kuidhinishwa ili kurejesha uhusiano na Pyongyang.

Jake Sullivan atakutana na Katibu Mkuu wa Usalama wa Kitaifa wa Japani Shigeru Kitamura na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Korea Kusini Suh Hoon katika Chuo cha Naval huko Annapolis, Md., Ikulu imesema.