MAREKANI

Marekani: Afisa wa polisi auawa katika shambulio Capitol Hill

Mtuhumiwa alijaribu kwanza kuwashambulia maafisa wa polisi na gari lake kabla ya kutoka kwenye gari lake na kuwashambulia kwa kisu Ijumaa Aprili 2 katika makao makuu ya Bunge la Marekani.
Mtuhumiwa alijaribu kwanza kuwashambulia maafisa wa polisi na gari lake kabla ya kutoka kwenye gari lake na kuwashambulia kwa kisu Ijumaa Aprili 2 katika makao makuu ya Bunge la Marekani. REUTERS - TOM BRENNER

Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na majengo ya bunge nchini Marekani Capitol huko Washington baada ya wagonga maafisa wawili wa polisi na gari lake na kisha kuwashambulia kwa kisu.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja maafisa hao wa polisi amekufa kwa majeraha aliyoyapata kufuatia shambulio hilo.

Miezi mitatu baada ya kushambuliwa kwa majengo ya bunge nchini Marekani kando na hotuba ya Donald Trump, makaomakuu ya Bunge la Marekani yalikumbwa tena na kisa kingine shambulio, Ijumaa hii, Aprili 2.

Shambulio hilo lilitokea pembezoni mwa jengo hilo la Bunge na lililenga vikosi vya usalama, na kusababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi.

"Mtuhumiwa aligonga mafisa wetu wawili na gari lake," kabla ya kugonga kizuizi, mkuu wa polisi katika mji wa Washington Capitol Yogananda Pittman amewaambia waandishi wa habari. "Wakati huo, mtuhumiwa alitoka kwenye gari lake na kisu mkononi" na "akaanza kuelekea kwa maafisa wa polisi wa Capitol", na baada ya hapo maafisa "wakampiga" risasi, amesema. Mmoja wa maafisa wawili waliojeruhiwa "alifariki," ameongeza. Aliyefanya shambulio hilo aliuawa kwa kupigwa risasi.

Shambulio hili halionekani kuhusishwa na "ugaidi", polisi imesema.