MAREKANI

Kesi ya mauaji ya Floyd: Mkuu wa Polisi wa Minneapolis amkabili Derek Chauvin

Mkuu wa Jeshi la Polisi katika mji wa Minneapolis nchini Marekani Medaria Arradondo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi katika mji wa Minneapolis nchini Marekani Medaria Arradondo. STR POOL VIA COURT TV/AFP

Mkuu wa Jeshi la Polisi katika mji wa Minneapolis nchini Marekani Medaria Arradondo  amesema hatua ya aliyekuwa afisa wa polisi Derek Chauvin ya kumbana shingoni kwa goti Mmarekani mweusi George Floyd, ilikuwa kinyume na mafunzo na sera ya jeshi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Arradondo ameyasema hayo katika kesi dhidi ya polisi huyo mzungu ambaye kitendo chake kilisababisha kifo cha Floyd na kuzua maandamano makubwa nchini Marekani na kwingineko duniani, mwezi Mei mwaka uliopita.

Ushuhuda huo ni wa kipekee na wa aibu sana kwa Derek Chauvin, siku ya sita ya kesi ya afisa huyo wa zamani wa polisi anayeshtakiwa kwa mauaji ya George Floyd. Medaria Arradondo amebaini kwamba afusa wake wa zamani alikiuka kabisa sheria za utumiaji wa nguvu  zinazotumika nkatika polisi ya manispaa.

Kesi dhidi ya polisi huyo Mzungu inatarajiwa kuendelea kwa angalau mwezi mmoja.