MAREKANI

Joe Biden: Watu wazima wote kuendelea kupata chanjo hadi Aprili 19

Rais wa Marekani Joe Biden Biden katika ikulu ya White House, Aprili 6, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden Biden katika ikulu ya White House, Aprili 6, 2021. AP - Evan Vucci

Rais wa Marekani Joe Biden ameongeza muda wa watu wazima kupokea chanjo ya Kwanza, kupambana na janga la Covid-19 kufikia Aprili 19.

Matangazo ya kibiashara

Biden katika hatua nyingine, ameonya kuwa taifa hilo bado lina safari ndefu ya kushinda vita dhidi ya virusi hivyo ambavyo vimeendelea kuwaaambukiza mamilioni ya watu nchini humo.

Joe Biden ameamuru majimbo yote ya Marekani kungeza muda unaostahiki wa chanjo kwa watu wazima wote ifikapo Aprili 19, wiki mbili kabla ya tarehe ya mwisho ya Mei 1 kutangazwa mwezi uliopita.

Kwa sehemu kubwa, majimbo ya nchi hiyo tayari yalikuwa yamebaini kwamba wamepanga kufungua kampeni ya kutoa chanjo hiyo kwa watu wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi kufikia tarehe hii mpya.

Rais wa Marekani pia amesema kuwa zaidi ya 80% ya waalimu na wafanyakazi wa shule mbalimbali nchini Marekani wamepata angalau dozi moja ya chanjo.