MAREKANI

Biden kuchukua hatua dhidi ya silaha zinazosababisha maafa Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden, Aprili 7, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden, Aprili 7, 2021. © REUTERS - KEVIN LAMARQUE

Rais wa Marekani Joe Biden atatangawza hatua za kwanza za utawala wake kuzuia vurugu za silaha leo Alhamisi, ikiwa ni pamoja na mpango wa kuzuia kuenea kwa silaha.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya matukio kadhaa ya  mauaji kwa kutumia silaha, hali hiyo imemlazimu sasa rais wa Marekani kuchukua hatua.

Joe Biden atatangaza kwamba wizara ya Sheria inakusudia kutoa kanuni inayopendekezwa ndani ya siku 30 kusaidia kupunguza kiwango cha "silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria" ambazo haziwezi kufuatiliwa, afisa wa Ikulu ya White House amesema. Maelezo ya kanuni hizi hayakuwekwa wazi mara moja.

Wizara pia itatoa mapendekezo ya sheria ndani ya siku 60 ili kufafanua kwamba vifaa ambavyo vinageuza bastola kuwa bunduki ya kivita vitakuwa chini ya Sheria ya Kitaifa inayohusu Silaha, ambayo inahitaji usajili wa silaha, afisa huyo amengeza.

Utata kuhusu udhibiti wa silaha Marekani

Udhibiti wa bunduki ni suala linalozua utata nchini Marekani, ambayo inashuhudia matukio mabaya ya mauaji yanayosababishwa na silaha kwa miongo kadhaa. Marekebisho ya Pili ya Katiba ya Marekani yanalinda haki ya kumiliki silaha.

Utawala wa Biden umekuwa ukifanya kazi kwa miezi kadhaa juu ya hatua za kudhibiti bunduki ambazo zinaweza kupunguza machafuko bila kusababisha vita vya kisheria ambavyo vinaweza kusababisha mahakama kuondoa sera hizo haraka.

Mpango wa nyuklia wa Iran: Nchi zenye nguvu zakutana na Marekani na Iran