MAREKANI

Daktari mchunguzi: George Floyd alifariki kutokana na kukamatwa kwake

Derek Chauvin anatuhumiwa kumuua George Floyd mnamo Mei 25, 2020 kwa kushikilia goti lake kwenye shingo ya Mmrekani huyo Mweusi kwa karibu dakika kumi kumzuia asifurukuti.
Derek Chauvin anatuhumiwa kumuua George Floyd mnamo Mei 25, 2020 kwa kushikilia goti lake kwenye shingo ya Mmrekani huyo Mweusi kwa karibu dakika kumi kumzuia asifurukuti. Angela Weiss AFP

Tatizo la moyo na utumiaji wa dawa za kulevya kwa George Floyd sio "sababu za moja kwa moja" za kifo chake, ambacho kilisababishwa na vurugu za kukamatwa kwake, daktari mchunguzi ambaye alifanya uchunguzi wake amesema akitoa ushahidi mahakamani Ijumaa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Katika mwisho wa wiki ya pili ya kesi ya polisi Mzungu Derek Chauvin, anayeshtumiwa kwa mauaji ya Mmarekani huyo Mweusi, taarifa hii inanakinzana na kauli iyotolewa na upande wa utetezi wa afisa huyo wa zamani wa polisi wa Minneapolis.

Anatuhumiwa kumuua George Floyd mnamo Mei 25, 2020 kwa kushikilia goti lake kwenye shingo ya Mmrekani huyo Mweusi kwa karibu dakika kumi kumzuia asifurukuti.

George Floyd alipiga kelele mara kadhaa "siwezi kupumua" kwa polisi hao watatu ambao walimuangusha kifudifudi kwenye barabara ya lami, mikono yake ikiwa imefungwa nyuma ya mgongo, wakimbana mgongoni, shingoni na kwenye mbavu.

Mapema wiki hii Mkuu wa Jeshi la Polisi katika mji wa Minneapolis nchini Marekani Medaria Arradondo  alisema hatua ya aliyekuwa afisa wa polisi Derek Chauvin ya kumbana shingoni kwa goti Mmarekani mweusi George Floyd, ilikuwa kinyume na mafunzo na sera ya jeshi hilo.