IRAN

Mvutano waibuka kati ya Marekani na Iran kuhusu vikwazo

Rais wa Iran Hassan Rouhani.
Rais wa Iran Hassan Rouhani. - Iranian Presidency/AFP

Maafisa wa Marekani na Iran wamevutana kuhusu vikwazo gani Washington inapaswa kuondoa ili kuanza kuheshimu mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015, na Washington ikibaini huenda hali ikawa ngumu zaidi ikiwa Tehran itashikilia madai ya kuondoa vikwazo vyote vya tangu 2017.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimechukua msimamo wakati mazungumzo ya moja kwa moja huko huko Vienna juu ya jinsi ya kurudisha nchi hizo mbili katika utekelzaji wa makubaliano yaliyomalizika kwa wiki moja sasa, na baadhi ya wajumbe wakisema kuna maendeleo.

Mazungumzo hayo, ambayo wawakilishi wa Umoja wa Ulaya wanasuluhisha pande hizo katika mkataba huo.

Marekani inataka Iran isitishe mpango wake wa kurutubisha uranimu, huku Iran ikitaka kwanza Marekani iondowe vikwazo vyake.