Ecuador: Lasso aibuka mshindi katika uchaguzi wa urais

Rais mteule wa Ecuador, Guillermo Lasso.
Rais mteule wa Ecuador, Guillermo Lasso. Fernando Mendez AFP

Guillermo Lasso ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ecuador dhidi ya mchumi kutoka mrengo wa kushoto Andres Arauz, hali ambayo inaashiria kuendelea kwa sera za kufungua masoko badala ya kurudi kwenye sera za kisochalisti katika nchi  hii ya Amerika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu iliyochapishwa na Tume ya Uchaguzi Uchaguzi, Guillermo Lasso amekuwa anaongoza kwa 52.5% baada ya kuhesabu 97% ya kura, dhidi ya mpinzani wake Andres Arauz (47.5%) ya kura , ambaye amekiri kushindwa.

Andres Arauz amewaambia wafuasi wake kwamba atampigia simu mpinzani wake kumpongeza kwa ushindi wake katika uchaguzi huo wa urais.

Akiongea mbele ya umati wa wafuasi wakiimba "Rais Lasso!" Guillermo Lasso amesema wananchi wa Ecuador "walitumia kura yao kuelezea mahitaji yao ya mabadiliko na hamu ya kuwa na maisa mazuri".

Guillermo Lasso ataapishwa Mei 24 kumrithi Lenin Moreno, ambaye hakuwania katika uchaguzi huo.