MAREKANI

Vurugu zaibuka Brooklyn Center baada ya mtu mweusi kupigwa risasi na polisi

Maafisa wa polisi wanaolinda makao makuu ya Polisi huko Brooklyn Center wakijaribu kuwatawanya waandamanaji, Minnesota, Marekani, Aprili 11, 2021.
Maafisa wa polisi wanaolinda makao makuu ya Polisi huko Brooklyn Center wakijaribu kuwatawanya waandamanaji, Minnesota, Marekani, Aprili 11, 2021. REUTERS - NICHOLAS PFOSI

Polisi wa Kituo cha Brooklyn imetumia gesi ya kutoa machozi kutawanya umati wa waandamanaji waliokuwa wakiandamana baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi mtu mweusi katika mji huo maili kumi kutoka Minneapolis, ambapo George Floyd aliuawa mwezi Mei mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Karibu watu 100, baadhi wakiwa na hasira na mmoja alikuwa ameshikilia bango lililoandikwa "George Floyd atendewe haki", walikabiliana na polisi wa ghasia baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi mtu mweusi aliyekuwa akiendesha gari lake.

Waandamanaji wengine waliharibu magari mawili ya polisi. Polisi kisha walifyatua risasi za mpira, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la REUTERS.

Usiku, waandamanaji zaidi ya mia moja walikusanyika mbele ya makao makuu ya polisi, ambayo ilikuwa inalindwa na maafisa zaidi ya mia moja wakiwa wamevalia sare zao. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya umati hu wa watu.

Kulingana na gazeti la Star Tribune, mtu aliyepigwa risasi anajulikana kwa jina la Daunte Wright,  mwenye umri wa miaka 20.

Meya wa Brooklyn atoa wito wa amani

Polisi wa Brooklyn Center imesema katika taarifa kwamba maafisa walisimamisha gari kwa ukiukaji wa sheria za barabarani kabla ya saa 2:00 usiku na kugundua kuwa dereva wa gari ilo alikuw anasakwa na mahakama.

Meya wa Brooklyn Center Mike Elliott amekiita kitendo hicho cha ufyatuaji risasi kuwa "kibaya". "Tunatoa wito kwa waandamanaji kuandamana kwa amani na kwamba waandamanaji wa amani hawakabiliani na vikosi vya usalama," amesema katika taarifa.