MAREKANI

Joe Biden atoa wito kwa utulivu baada ya kifo cha kijana mweusi Minneapolis

Meya wa Minneapolis amesema vikosi vya usalama na kikosi cha walinzi taifa wa Minnesota watatumwa kwa idadi kubwa katika eneo linalokabiliwa na vurugu.
Meya wa Minneapolis amesema vikosi vya usalama na kikosi cha walinzi taifa wa Minnesota watatumwa kwa idadi kubwa katika eneo linalokabiliwa na vurugu. AP - Jim Mone

Sheria ya kutotoka nje usiku imetangazwa tangu Jumatatu huko Minneapolis baada ya makabiliano yaliyofuatia kifo cha kijana Mmarekani mweusi, Daunte Wright, aliyeuawa siku moja kabla na afisa wa polisi.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden amehuzunishwa na kifo cha "kutisha" wakati akitoa wito kwa waandamanaji kuwa "watulivu na kufanya maandamano yao kwa amani".

"Kilichotokea ni cha kusikitisha sana, lakini nadhani tunapaswa kusubiri na kuona nini uchunguzi unatuambia," amesema Joe Biden baada ya makabiliano yaliyofuatia kifo cha Daunte Wright katika Kituo cha Brooklyn, kitongoji cha Minneapolis. "Kwa sasa, nataka kusema tena wazi: hakuna haki yoyote, utetezi wowote kwa uporaji," ameaongeza.

"Maandamano ya amani yanaeleweka," amebaini Joe Biden. "Na ukweli ni kwamba, tunajua kwamba hasira, maumivu, mateso ambayo yapo kwa watu weusi katika muktadha huu, ni ya kweli, makubwa na muhimu." "Lakini hiyo haimaanishi vurugu," amesisitiza.

Meya wa Minneapolis Jacob Frey ametangaza sheria ya kutotoka nje usiku katika eneo hilo, kuanzia saa moja usiku hadi saa 12 asubuhi. Itatumika pia huko St-Paul, mji pacha wa Minneapolis, na katika kaunti tatu za eneo la mji mkuu, amesema meya wa St-Paul na gavana wa Minnesota. Vikosi vya usalama vya Minnesota vitatumwa kwa idadi kubwa, amesema Jacob Frey. Kulingana na mamlaka, karibu askari 500 wa kikosi cha Walinzi wa kitaifa tayari wapo kaika eneo hilo.