MAREKANI

Mwanafunzi auawa kwa risasi na polisi huko Tennessee

Maafisa wa polisi wakabiliana na mfalifu katika shule ya upili huko Knoxville, Tennessee, Marekani.
Maafisa wa polisi wakabiliana na mfalifu katika shule ya upili huko Knoxville, Tennessee, Marekani. via REUTERS - Brianna Paciorka/News Sentinel

Polisi huko Knoxville, Tennessee, wamempiga risasi mwanafunzi wa shule ya upili Jumatatu wiki hii baada ya kuwafyatulia risasi maafisa shuleni, na kumjeruhi mmoja wa maafisa hao.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo, ambalo lilifanyika karibu saa 9:15 alaasiri kwa katika shule ya Austin-East Magnet, linaongeza orodha ya visa vya mauaji ya watu wengi kwa kutumia bunduki. Matukio ambayo yamefanyika kote Marekani tangu katikati ya mwezi Machi.

Polisi wa Knoxville inasema afisa huyo liyejeruhiwa kwa risasi anapewa matibabu, wana imani kuwa atapona. Alipigwa risasi mguuni.

Polisi waliwenda huko Austin-Mashariki baada ya kuarifiwa kuwa mtu mwenye bunduki alikuwa katika shule hiyo. Mshukiwa alikuwa alikuwa amejificha bafuni, ambapo urushianaji risasi ulitokea.