MAREKANI

Marekani: Wademocrats wafichua muswada wa kurekebisha Mahakama Kuu

Makao makuu ya Bunge nchini Marekani.
Makao makuu ya Bunge nchini Marekani. Joe Raedle POOL/AFP

Wabunge kutoka chama cha Democraticnchini Marekani wanapanga kuwasilisha muswada bungeni leo Alhamisi kuhusu kuongeza majaji wanne kwenye Mahakama Kuu ya Marekani, pendekezo linalokusudiwa kuvunja udhibit wa Warepublican kwenye mahakama hiyo, hali ambayo inaonekana italeta upinzani mkali kutoka Republican

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo itaongeza idadi ya majaji kutoka tisa hadi kumi na tatu, kulingana na nakala ya muswada wa Seneti ambayo shirika la habari la REUTERS limepata kopi.

Siku ya Ijumaa ya iki iliyopita Rais Joe Biden alitangaza kuundwa kwa tume ya pande mbili itakayohusika na kujadili mabadiliko yanayowezekana kwenye Mahakama Kuu, ikiwa ni pamoja na kupanua au kuweka kikomo kwa idadi ya mihula ya majaji badala ya uteuzi wa sasa wa milele.

Idadi ya majaji katika Mahakama Kuu yaongezwa Marekani

Kumekuwa na majaji tisa wa Mahakama Kuu tangu mwaka 1869, lakini Baraza la Congress lina uwezo wa kubadilisha idadi, jambo ambalo tayari limefanya mara kadhaa kabla ya tarehe hiyo.

Rais wa zamani wa kutoka chama cha Republican Donald Trump aliweza kuteua majaji watatu wakati utawala wake wa miaka miaka minne, akiipa korti idadi kubwa ya Wahafidhina 6 dhidi ya 3

Jaribio la mwisho la kurekebisha Mahakama Kuu lilianzia miaka ya 1930. Rais Franklin D. Roosevelt alitafuta kuongeza idadi ya majaji bila mafanikio baada ya mfululizo wa maagizo yasiyofaa kwa baadhi ya hatua zake.