MAREKANI

Marekani: Watu wasiopungua 8 wauawa kwa kupigwa risasi Indianapolis

Several people have been shot in an incident in Indianapolis, police say
Several people have been shot in an incident in Indianapolis, police say SPENCER PLATT GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/File

Tukio hilo lilitokea Alhamisi jioni wiki hii huko Indianapolis, katikati mwa Marekani. Miili ya wahanga hao ilipatikana katika kituo cha shirika la usafirishaji wa barua na vifurushi cha FedEx karibu na uwanja wa ndege wa jiji hilo, ambapo mtu mwenye bunduki alifyatua risasi, msemaji wa polisi amesema, shirika la habari la AFP limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengine wamelazwa hospitalini, polisi imeongeza bila kutaja idadi yao.

Mwanamume anayefanya kazi kwenye eneo hilo aameiambia televisheni ya WISH-TV katika mji huo kwamba aliona mtu mmoja akifyatua risasi hovyo na alisikia zaidi ya risasi kumi.

"Nilimwona mtu mmoja akiwa na aina fulani ya bunduki ndogo, na alifyatua risasi hovyo," Jeremiah Miller amesema. "Niliinama mara moja na niliogopa."

FedEx imethibitisha katika taarifa yake kutokea kwa shambulio hilo kwenye eneo lake na kubaini kwamba shirika hilo linashirikiana na mamlaka.

FedEx imethibitisha katika taarifa yake kutokea kwa shambulio hilo kwenye eneo lake na kubaini kwamba shirika hilo linashirikiana na mamlaka.
FedEx imethibitisha katika taarifa yake kutokea kwa shambulio hilo kwenye eneo lake na kubaini kwamba shirika hilo linashirikiana na mamlaka. AP - Steve Helber

Visa vya mauaji vyakithiri Marekani

Visa vya mauaji vinaendelea kushuhudiwa nchini Marekani wakati utawala wa Joe Biden umekuwa ukitafakari namna ya kukabiliana na umiliki wa silaha za kivita nchini humo.

Marekani ni moja ya nchi chache duniani kuruhusu raia kumiliki silaha kwa lengo la kujihami, kutokana na makundi ya kigaidi ambayo Marekani imekuwa ikikabiliana nayo katika nchi mbalimbali, hasa katika Mashariki ya Kati Somalia na Afrika Magharibi.