CUBA

Ukurasa wa historia wageuka Cuba: Raul Castro kuachia ngazi

Mkuu wa Chama cha Kikomunisti nchini Cuba Raul Castro (kushoto) akisalimiana na Rais Miguel Diaz-Canel wakati wa kufunga mkutano wa Bunge la kitaifa la nchi hiyo.
Mkuu wa Chama cha Kikomunisti nchini Cuba Raul Castro (kushoto) akisalimiana na Rais Miguel Diaz-Canel wakati wa kufunga mkutano wa Bunge la kitaifa la nchi hiyo. AFP

Katika siku chache, Fidel Castro hatakuwa tena madarakani nchini Cuba: kongamano la Chama cha Kikomunisti, ambalo litafunguliwa leo Ijumaa, litasitisha miongo sita ya utawala wa kidugu ambao sasa unaachia kizazi kipya nafasi.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kifo cha Fidel Castro mnamo mwaka 2016, kustaafu kwa Raul, ambaye hivi karibuni atatimiza umri wa miaka 90, ambaye alimkabidhi kijiti cha uongozi wa nchi Rais Miguel Diaz-Canel, 60, ukurasa wa kihistoria kwa kisiwa hicho na wakaazi wake unabadilika, ambapo karibu wakaazi wote wa Cuba hawaijui familia yoyote katika uongozi wa nchi hiyo kuliko ile ya wanamapinduzi maarufu.

"Raul hatakuwa kiongozi wa chama tena, lakini ikiwa kuna tatizo Raul atakuwepo, hajafa", Ramon Blande, mwanaharakati wa kikomunisti, 84, amesema.

Na kwa kweli, Miguel Diaz-Canel "bado ni kijana", lakini " kwa kweli anakabiliwa na matatizo mbalimbali", ameongeza.

Kuanzia saa 3:00 asubuhi (sawa na saa7:00 mchana ), wajumbe zaidi ya mia moja wa chama kimoja, kutoka majimbo yote, watakutana kwa siku nne katika mji mkuu, kwenye vikao mbalimbali, kujadili maswala makubwa ya nchi.

Uteuzi wa Bwana Diaz-Canel kama katibu mpya wa kwanza, wadhifa muhimu zaidi nchini Cuba, unatarajiwa kufanyika siku ya mwisho, Jumatatu.