HAITI

Haiti: Watatu kati ya viongozi saba waliotekwa nyara waachiliwa

Kanisa la St Rock ambapo kasisi wa Ufaransa, ambaye alitekwa nyara Jumapili pamoja na makasisi wengine, Port-au-Prince, Haiti Aprili 12, 2021.
Kanisa la St Rock ambapo kasisi wa Ufaransa, ambaye alitekwa nyara Jumapili pamoja na makasisi wengine, Port-au-Prince, Haiti Aprili 12, 2021. REUTERS - Valerie Baeriswyl

Watatu kati ya Mapadri watano na watawa wawili wa kike waliotekwa nyara nchini Haiti siku zaidi ya kumi zilizopita wameachiliwa, amesema msemaji wa Baraza kuu la Maaskofu la taifa hilo la Caribea linalozidi kugubikwa na matukio ya utekaji nyara na uhalifu wa vurugu.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa kidini, wakiwemo raia wawili wa Kifaransa, walitekwa katika eneo la Croix-des-Bouquets, kaskazini-mashariki mwa mji mkuu Port-au-Prince, kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama cha muungano wa kidini CHR, Father Gilbert Peltrop.

"Watatu kati ya viongozi saba wa kidini waliotekwa nyara Aprili 11 wameachiliwa," Padri Loudger Mazile ameliambia shirika la habari la AFP. "Lakini raia wawili kutoka Ufaransa bado wanashikiliwa matekai. Hakuna watu wa kawaida kati ya wale walioachiliwa," ameongeza.

Watekaji nyara walikuwa wanaomba fidia ya dola milioni moja ili wawezekuwaachilia mateka hao.

Kundi la 400 Mawozo lashukiwa kuhusika na utekaji nyara

Watu watatu, kutoka familia wa kasisi wa Haiti ambaye hakuwa miongoni mwa waliotekwa nyara, pia walitekwa nyara. Asilimia kubwa ya raia wa Haiti ni Wakatoliki na nchi yao ni masikini zaidi katika bara la Amerika.

Polisi wanashuku genge lenye silaha katika eneo hilo, lililopewa jina la "400 Mawozo", kuwa linahusika na utekaji nyara huo, kulingana na chanzo cha kuaminika.

Utekaji huo umekuja chini ya wiki mbili tangu watu wenye silaha walipomteka mchungaji wa Kihaiti na wengine watatu katika tukio lililorushwa mubashara kwenye ukurasa wa Facebook