COLOMBIA

Colombia yakumbwa na maandamano kupinga marekebisho ya kodi

Waandamanaji wakikusabyika wakati wa maandamano ya kupinga mageuzi ya sheria za kodi yaliyopendekezwa na serikali ya Ivan Duque, Bogota, Aprili 28, 2021.
Waandamanaji wakikusabyika wakati wa maandamano ya kupinga mageuzi ya sheria za kodi yaliyopendekezwa na serikali ya Ivan Duque, Bogota, Aprili 28, 2021. REUTERS - LUISA GONZALEZ

Maelfu ya waandamanaji wameitikia wito kutoka kwa vyama vikubwa vya wafanyakazi nchini Colombia kuingia mitaani Jumatano wiki kupinga muswada wenye utata wa marekebisho ya kodi.

Matangazo ya kibiashara

Watu arobaini walikamatwa kwa tuhuma za uharibifu, serikali imesema, na maafisa 42 wa polisi walijeruhiwa. Polisi walitumia mabomu ya machozi katika miji mikubwa ambapo visa kadhaa vya machafuko vilizuka.

Huko Bogota, maafisa 31 wa polisi na raia walijeruhiwa, kulingana na manispaa ya jii. Jiji la Cali magharibi mwa nchi, liliuma jeshi na kutangaza sheria ya kutotoka nje saa 7 mchana baada ya mabasi kadhaa kuchomwa moto.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamano mengine leoAlhamisi na kutangaza maandamano mengine Mei 19.

"Tunamuomba Rais Duque aondoe marekebisho ya kodi," Francisco Maltes, kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi cha Kati (CUT), amesema katika mkutano na waandishi wa habari.