BRAZILI

Coronavirus: Idadi ya vifo kutokana na COVID -19 yakaribia 400,000 Brazil

Mgonjwa aliye wa Covid-19 akisafirishwa kwa ndege ya jeshi katika uwanja wa ndege wa Manaus katika Amazon ya Brazil Januari 15, 2021.
Mgonjwa aliye wa Covid-19 akisafirishwa kwa ndege ya jeshi katika uwanja wa ndege wa Manaus katika Amazon ya Brazil Januari 15, 2021. AFP - MICHAEL DANTAS

Brazil inatarajia kurekodi vifo vya 400,000 wiki hii kutokana na COVID-19, baada ya wizara ya afya siku ya Jumatano kuripoti vifo vipya 3,163 kutokana na COVID-19  kati ya kipindi cha saa 24, na kusababisha idadi rasmi ya vifo kfikia 398,185.

Matangazo ya kibiashara

Brazil inatarajia kufikisha idadi kubwa ya vifo duniani, sawa na ile ya Marekani, ambayo imerekodi zaidi ya vifo  570,000 kwa jumla.

Mgogoro wa COVID-19 nchini Brazil ulishindwa kudhibitiwa katika miezi ya hivi karibuni, pamoja na vizuizi visivyo halali kuhusu watu kutembea na aina mpya ya kirusi cha Corona kinachoambukia haraka.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amekosolewa vikali kwa kudharau hatari za virusi, kwa kupuuzia uvaaji wa barakoa na kupendekeza tiba ambazo hazijathibitishwa.

Wizara ya afya ya Brazil pia imeripoti visa vipya 79,726 vya maambukizi vilivyothibitishwa siku ya Jumatano, na kufanya jumla visa vya maambukizi kufikia 14,521,289.