MAREKANI

Marekani: Wahamiaji zaidi ya 90 wapatikana wamefungiwa katika nyumba Houston

Wahamiaji wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Mexico na Marekani huko Ciudad Juarez, Machi 23, 2021 (Picha ya kumbukumbu).
Wahamiaji wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Mexico na Marekani huko Ciudad Juarez, Machi 23, 2021 (Picha ya kumbukumbu). AP - Christian Chavez

Wahamiaji zaidi ya 90 wamepatikana wamefungiwa katika nyumba moja huko Houston, mwendo wa saa tano kwa gari kutoka mpaka wa Mexico na Marekani. 

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mamlaka ya Texas, biashara hii ya binadamu inaendana na visa vya watu kuingia kinyume ch sheria nchini Marekani, ambavyo walinzi wa mpaka wanakabiliwa navyo karibu kila siku katika jimbo hilo.

Maafisa wa polisi wamefaulu kusitish biashara hiyoharamu ya kibinadamu. Walikuwa na waranti kuhusiana na visa hivi vya utekaji nyara, walipokutana na wahamiaji karibu 100 wamefungiwa katika nyumba hiyo huko Houston.

Wahamiaji walikuwa wamepungukiwa maji mwilini

Katika mtaa huu wa kusini mwa mji wa Houston unaokaliwa zaidi na wastaafu, maafisa wa polisi wamegundua wahamiaji hao ambao walikuwa wamepungukiwa kwa kiasi kikubwa maji mwilini na walikuwa hawajala kwa siku kadhaa, wengi wao walishindwa kusimama kwa kukosa nuvu. Baadi yao walikuwa na dalili za maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, angalau watano wamepatikana na ugonjwa huo.

Mwanafamilia wa mmoja wa wahamiaji waliopatikana katika nyumba hiyo alikuwa amewaarifu polisi.