MAREKANI

COVID-19 Marekani: Mamlaka yatiwa wasiwasi kuona dozi ya pili ya chanjo yapuuzwa

CDC inasema 8% ya Wamarekani wamepuuzia dozi ya pili ya chanjo.
CDC inasema 8% ya Wamarekani wamepuuzia dozi ya pili ya chanjo. © Getty Images via AFP - MATTHEW HATCHER

Nchini Marekani, ambapo dozi milioni 243 zimetolewa, zaidi ya 30% ya raia wamepewa chanjo kamili na 55% wamechanjwa sindano ya kwanza. Lakini mamlaka ina wasiwasi kuwa 8% ya wale ambao tayari wamepokea dozi ya kwanza wamepuuzia dozi ya pili ya chanjo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza (CDC), zaidi ya watu milioni 5 hawakujitokeza kwa dozi ya pili ya chanjo. CDC inaeleza kuwa kuna sababu kadhaa za jambo hili. Baadhi ya Wamarekani wanasema wanaogopa athari za chanjo ya pili ambayo inaweza kuwa kali zaidi kuliko dozi ya kwanza, kama homa, maumivu ya misuli au maumivu ya kichwa.

Wengine wanasema wanahisi kuwa watakuwa salama na dozi moja tu na hawaoni haja ya kupata chanjo ya pili.

Maafisa wa CDC pia wamegundua kuwa katika baadhi ya visa hususan suala la upatikanaji wa chanjo ambalo liko mashakani. Mtu ambaye amepokea dozi ya chanjo ya Pfizer, kwa mfano, wakati mwingine anapata usumbufu wa kupata mahali ambapo chanjo kama hiyo inapatikana ili apate dozi ya pili ya chanjo.