MAREKANI

Joe Biden aongeza idadi ya wakimbizi wanaotakiwa Marekani kila mwaka

Wahamiaji wakijaribu kuvuka ukuta wa mpaka kinyume cha sheria kwenda Marekani huko Tijuana, Mexico.
Wahamiaji wakijaribu kuvuka ukuta wa mpaka kinyume cha sheria kwenda Marekani huko Tijuana, Mexico. REUTERS/Adrees Latif

Kizingiti hiki kilikuwa kimepunguzwa hadi chini kabisa na Donald Trump. Katika wiki za hivi karibuni, taarifa zinazokinzana za Joe Biden juu ya kizingiti hiki zimesababisha upinzani mkali katika kambi yake mwenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hii ilikuwa imepunguzwa hadi chini kabisa na Donald Trump. Katika wiki za hivi karibuni, taarifa zinazopingana na Joe Biden juu ya kizingiti hiki zimempa upinzani mkali katika kambi yake mwenyewe.

Rais wa Marekani Joe Biden ameamua kuongeza hadi 62,500 idadi ya wakimbizi wanaoweza kukubaliwa kwa muda kuishi nchini Marekani kwa mwaka huu, baada ya kukosolewa vikali kutokana na uamuzi huo.

Uamuzi huu, uliosubiriwa kwa hamu katika kambi ya Wademocrats, unamuwezesha, siku 100 baada ya kuingia madarakani, ili kumaliza tofauti na mtangulizi wake Donald Trump, ambaye alikuwa ameweka kizingiti cha chini kihistoria cha watu 15,000 ambao wanaruhusiwa kupokelewa nchini Marekani kama wakimbizi.

Wakimbizi 125,000 kukubaliwa mwaka ujao

Kwa mwaka ujao, Joe Biden ametangaza kizingiti cha wakimbizi 125,000, huku akisisitiza kwamba lengo hilo, kama hili la mwaka huu, litakuwa ngumu kutimiza kwa sababu ya haja ya "kuunda upya mpango wa uandikishaji wa wakimbizi.

"Tunafanya kazi kwa bidii kurekebisha uharibifu wa miaka minne iliyopita," amesema katika taarifa.

Mpango huu unahusu tu wakimbizi waliochaguliwa na vyombo vya usalama na ujasusi vya Marekani katika kambi za Umoja wa Mataifa duniani kote ili kupatiwa makazi nchini Marekani, hasa kati ya walio hatarini zaidi.