UKRAINE-DIPLOMASIA

Marekani: Blinken azuru Ukraine, ishara ya uungwaji mkono

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anashuka ndege kwenye uwanja wa ndege wa Boryspil nje ya mji wa Kiev, Ukraine, mwanzo wa ziara ya siku moja.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anashuka ndege kwenye uwanja wa ndege wa Boryspil nje ya mji wa Kiev, Ukraine, mwanzo wa ziara ya siku moja. Efrem Lukatsky POOL/AFP

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amefanya ziara mjini Kiev Alhamisi hii ambapo anatarajiwa kukutana na Rais Volodimir Zelensky, baada ya kutoa wito kwa Ukraine kuanza njia ya mageuzi na vita dhidi ya ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Aprili Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi kumsaidia Rais Volodimir Zelensky, wakati Urusi ililipeleka wanajeshi kwenye mpaka na nchi hiyo na katika eneo la Crimea linalokaliva kimabavu na Urusi.

Moscow ilitangaza kuondoa vikosi vyake Aprili 22, ikitengeneza njia ya mkutano kati ya Joe Biden na Rais wa Urusi Vladimir Putin ambao unaweza kufanyika mapema mwezi Juni.

Mvutano huo ulisababisha Ukraine kuomba Marekani na Ulaya kusaidia kuharakisha kuingia kwa Kiev katika muungano wa kijeshi wa NATO.

"Tunachukulia ziara hii kama ishara kubwa ya uungwaji mkono kutoka Marekani kukabiliana na uchokozi wa Urusi," Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine Yevhenii Yenin amesema kabla ya Anthony Blinken kuwasili Ukraine.

Washington ndiye msaidizi mkubwa wa Kiev tangu Urusi ilipounganisha Crimea mnamo mwaka 2014 na kuzuka kwa mzozo wa Donbass kati ya wanajeshi wa Ukraine na vikosi vinavyotaka maeneo yao kujitawala vinavyoungwa mkono na Urusi ambavyo Kiev inasema viliua watu 14,000 kwa kipindi cha miaka saba.