MAREKANI-AFYA

Marekani: Watu waliopewa chanjo kamili wanaweza kuondoa barakoa

Wamarekani waliopewa chanjo dhidi ya COVID-19 hawahitaji tena kuvaa barakoa nchini humo, maafisa wa afya wamesema Alhamisi.
Wamarekani waliopewa chanjo dhidi ya COVID-19 hawahitaji tena kuvaa barakoa nchini humo, maafisa wa afya wamesema Alhamisi. Kena Betancur AFP/File

Watu waliopewa chanjo kamili dhidi ya COVID-19 hawaitaji kuvaa barakoa nje na wanaweza kuepuka kuzivaa ndani ya nyumba katika maeneo mengi, mamlaka ya vituo vya Kudhibiti na Kuzuia magonjwa ya maambukizi nchini Marekani (CDC) imesema.

Matangazo ya kibiashara

Pia hawaitaji kutii sheria za kutokaribiana na mtu mwengine isipokuwa kwa watu wachache, CDC imeongeza, ikisema inaamini miongozo hiyo inawapa matumaini Wamarekani kwa kwenda kupata chanjo.

Miongozo hiyo mipya inaonysha kwamba Wamarekani waliopewa chanjo wanaweza kuendelea na safari zao zote, hawaitaji kuwekwa karantini baada ya kusafiri katika nchi mbalimbali duniani, na hawaitaji kupimwa virusi vya COVID-19 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa virusi hivyo ambaye hana dalili yoyote.

Rais wa Marekani Joe Biden alitoka Ikulu na kuongea bila kuvaa barakoa. "Nadhani ni hatua kubwa, siku muhimu," amesema.

CDC, hata hivyo, inapendekeza kwamba wale waliopewa chanjo waendelea kuvaa barakoa zao kwenye ndege na treni, na pia kwenye viwanja vya ndege, usafiri wa umma, na hospitali au katika vituo vya matibabu.