BRAZILI

Meya wa Sao Paulo, Bruno Covas, aaga dunia

Meya wa Sao Paulo, Bruno Covas, amefariki dunia Jumapili hii Mei 16, akiwa na umri wa miaka 41, kwa saratani ya mfumo wa mmeng'enyo.
Meya wa Sao Paulo, Bruno Covas, amefariki dunia Jumapili hii Mei 16, akiwa na umri wa miaka 41, kwa saratani ya mfumo wa mmeng'enyo. NELSON ALMEIDA AFP/Archivos

Meya wa Sao Paulo, Bruno Covas, amefariki dunia Jumapili hii Mei 16, akiwa na umri wa miaka 41, kwa saratani ya mfumo wa mmeng'enyo ambayo aliugua tangu mwaka 2019, imesema katika taarifa hospitali ya mji mkuu wa uchumi wa Brazil, inayomilikiwa na nchi za watu kutoka Syria na Lebanoni, ambapo alikuwa akipewa huduma za matibabu.

Matangazo ya kibiashara

"Meya Bruno Covas amefariki leo saa 8:20 asubuhi kutokana na saratani (ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula) baada ya matibabu ya muda mrefu", imeelezea taarifa kutoka hospitalini.

Hali yake ilikuwa haiwezi kurekebishwa

Habari hiyo imezua sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo maelfu ya watu waliwasilisha rambi rambi zao na mshikamano na familia yake, hasa kwa mtoto wake Tomas, mwenye umri wa miaka 15. "Asante kwa Bruno Covas kwa kushiriki nasi sote na kutuonyesha mapenzi ya hati na kujitolea," Gavana wa mji wa Sao Paulo Joao Doria mesema katika taarifa.

Siku ya Ijumaa, timu ya matabibu iliyo kuwa ikimuhudumiwa Bruno Covas ilitangaza kuwa hali yake haiwezi kurekebishwa. Alikuwa amelazwa hospitalini Mei 2 baada ya kugundua kuwa anatokwa na damu katika matumbo wakati wa vipimo vya awali ili kuendelea na vipimo vingine.