MAREKANI

Marekani: Mazungumzo juu ya mpango wa miundombinu yakabiliwa na upinzani

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. Nicholas Kamm AFP

Mazungumzo juu ya mpango mkubwa kuhusiana na miundombinu nchini Marekani unaopendekewza na Joe Biden yanakumbana na upinzani kutoka kwa kambi ya Warepublican licha ya pendekezo la White House la kupunguza fedha zitakazotumiwa kwa mpango huo

Matangazo ya kibiashara

Kiasi fedha cha awali kilichopangwa kwa mpango huo, ambao rais wa Marekani alifanya moja ya vipaumbele vya mwanzo wa muhula wake, ilikuwa dola Bilioni 2,250 (sawa na euro Bilioni 1,843).

Siku ya Ijumaa, Ikulu ya White House ilipendekeza kupunguza kiwango hicho hadi dola Bilioni 1.7, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yaliyopangwa kwa mitandao ya mawasiliano, barabara na madaraja.

Kambi hizo mbili, hata hivyo, bado zinapingana kabisa, kwa jumla ya mpango na ufadhili wake.

Ikulu ya White House ilijaribu kupeleka mjadala mbele kwa kuwasilisha toleo lake jipya siku ya Ijumaa kwenye mkutano wa mkondoni na kundi la maseneta wa chama cha Republican.

"Pendekezo hili linaonyesha nia ya kupunguza kiwango cha matumizi ya mpango huo kwa kuhamisha katika tasnia zingine ambazo ni muhimu kwa rais [...] huku tukibaki makini kwa mambo muhimu zaidi kwa ujenzi wa baadaye wa miundombinu yetu na tasnia zetu,"Msemaji wa White House Jen Psaki amewaambia waandishi wa habari.

Matumizi mengine yaliyoondolewa kutoka kwa mpango mpya, hususan uwekezaji katika utafiti na maendeleo, unaweza kuwa katika miswada mingine, ameongeza.

Gharama ni kubwa kwa upande wa Republican

Kundi la maseneta wa chama cha Republican, ambao walikuwa wametoa pendekezo lao wenyewe, kwa kiwango kidogo sana, walisema pendekezo jipya la Ikulu ya White House haliwezi kupokelewa lakini wameonyesha nia yao ya kuendelea na mazungumzo.

Pendekezo jipya la utawala wa Biden linapunguza uwekezaji katika mitandao ya mkondoni hadi dola Bilioni 65 kutoka dola Bilioni 100 katika mpango wa awali, inaonyesha hati ya ndani ya White House.