MAREKANI-ISRAEL

Biden kumteua Thomas Nides kuwa balozi nchini Israeli

Rais wa Marekani Joe Biden azungumza na waandishi wa habari wakati anaondoka White House huko Washington, Marekani, Mei 25, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden azungumza na waandishi wa habari wakati anaondoka White House huko Washington, Marekani, Mei 25, 2021. REUTERS - KEVIN LAMARQUE

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumteua Thomas Nides, mwanadiplomasia mzoefu ambaye pia ameshikilia nyadhifa za juu katika sekta ya fedha, kuwa balozi wa Marekani nchini Israel, duru za kuaminika zimebaini leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Biden, uliowekwa tangu mwezi Januari, umekosolewa kwa kukosa kuteua uwakilishi wa kidiplomasia katika ngazi ya juu kabisa katika taifa la Kiyahudi wakati wa mzozo kati ya vikosi vya Israel kundi la wanamgambo wa Hamas, hali ambayo ilmesababisha Ikulu ya White House kuifanya faili hii kuwa kipaumbele cha juu.

Haijafahamlika ikiwa Joe Biden anapanga kutangaza mwenyewe uteuzi wa Thomas Nides, duru za kuaminika zinafahamisha kwamba uteuzi huo utakuwa rasmi mapema sana. Ikulu imekataa kutoa maelezo zaidi.

Thomas Nides, ambaye sasa ni mjumbe wa timu ya usimamizi wa Benki ya Morgan Stanley, alikuwa nibu waziri anayehusika na masuala ya Usimamizi na Rasilimali wakati wa utawa wa rais Barack Obama.

Mpinzani wake mkuu katika ubalozi wa Marekani nchini Israeli alikuwa Robert Wexler, mjumbe wa zamani wa Florida na mjuzi wa Mashariki ya Kati.