MAREKANI-AFYA

Joe Biden ataka ripoti ya kijasusi juu ya chimbuko la CoOVD-19 ndani ya siku 90

Rais wa Marekani ametoa wito kwa idara zote za ujasusi za nchi hiyo kuongeza juhudi zao kuelezea chanzo cha COVID-19.
Rais wa Marekani ametoa wito kwa idara zote za ujasusi za nchi hiyo kuongeza juhudi zao kuelezea chanzo cha COVID-19. Nicholas Kamm AFP/File

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa idara za ujasusi za Marekani "kuongeza juhudi zao" kupata chimbukolya COVID-19. nadharia ya ajali ya maabara huko Wuhan, nchini China, iliyopuuzwa na wataalam wengi, imerudi kwa nguvu katika wiki za hivi karibuni katika mjadala nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Katika wiki za hivi karibuni, Joe Biden alikuwa ameomba idara za ujasusi za Marekani kujibu swali linaloukabili ulimwengu wote: nini chimbuko la Corona? Je! COVID 19 imeambukizwa kwa njia ya kawaida kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu au, ni kutokana na ajali ya maabara nchini China?

Katika ripoti yao ya kwanza, idara za ujasusi nchini Marekani zilishindwa kupata majibu. Baada ya kutoridhika, Joe Biden amezitaka "wkuzidisha juhudi zao" na kwa hivyo amezipa siku 90 kutoa ripoti ya pili yenye ujumbe rasmi wa "kutuleta karibu na hitimisho la mwisho" juu ya hali hizi mbili ambazo White House inaona kuwa zinawezekana.

Shinikizo kwa China

Rais wa Marekani Joe Biden ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kutambuwa hasa chanzo cha maambukizi ya virusi vya corona, na kuitaka China kushirikiana na wachunguzi wa kimataifa kufanikisha mchakato huo.

Maafisa wengine wa Marekani wana mashaka makubwa juu ya nadharia ya virusi hivyo kuwa vimevujishwa kutoka kwenye maabara. Daktari Anthony Fauci, mshauri wa virusi vya corona katika Ikulu ya White House, amesema kwamba yeye na wanasayansi wengine wanaamini kuwa uwezekano mkubwa ni kwamba yalikuwa ni maamukizi ya kawaida, lakini hakuna mtu anayejua hakika kwa asilimia 100.

Ubalozi wa China nchini Marekani umeandika kwenye tovuti yake baada ya tamko hilo la Biden kwamba wazo la virusi hivyo kuvujishwa kutoka kwenye maabara ni nadharia isiyokuwa na ukweli.

Serikali ya China imesema kuingiza siasa katika kutafuta chanzo cha virusi vya corona kutazuia sana ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na janga hilo. Pia imesema kwamba China imeunga mkono utafiti ulioangalia kwa undani maambukizi ya awali ya virusi vya corona ulimwengu kote.