MAREKANI-USALAMA

Marekani: Wawili wauawa katika shambulio la risasi Florida

Gavana wa Jimbo la Florida Ron DeSantis akisafiri kwa ndege juu ya anga la pwani ya magharibi ya Florida.
Gavana wa Jimbo la Florida Ron DeSantis akisafiri kwa ndege juu ya anga la pwani ya magharibi ya Florida. AFP - HANDOUT

Angalau watu wawili wameuawa na karibu 20 wamejeruhiwa kwa risasi nje ya ukumbi wa tamasha huko Hialeah, Florida, nchii Marekani, mamlaka nchini humo imesema.

Matangazo ya kibiashara

"Niko kwenye eneo la la shambulio lililotekelezwa kwa silaha ya moto, kitendo kiovu, ambapo watu zaidi ya 20 wamejeruhiwa na wengine wawili wamepoteza maisha," mkuu wa polisi wa Kaunti ya Miami-Dade, Alfredo Ramirez III, ameandikakwenye Twitter.

Kulingana na kituo cha CNN, watu watatu waliokuwa wanaendesha gari aina ya SUV walifyatua risasi dhidi ya umati uliokusanyika mbele ya ukumbi wa tamasha.

Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana.