MAREKANI

Marekani: Bunge la Seneti lapitisha muswada kuhusu ushindani na China

Kiongozi wa wengi kutoka chama cha Dmocratic katika Bunge la  Seneti Chuck Schumer, ameonya juu ya athari mbaya za kutokuwa na ufadhili wa utafiti kushindana na China.
Kiongozi wa wengi kutoka chama cha Dmocratic katika Bunge la Seneti Chuck Schumer, ameonya juu ya athari mbaya za kutokuwa na ufadhili wa utafiti kushindana na China. JIM WATSON AFP/File

Bunge la Seneti Marekani Jumanne wiki hii liliidhinisha, kwa kura 68 dhidi ya 32, mlolongo mkubwa wa sheria inayolenga kuimarisha uwezo wa nchi kushindana na China, hasa katika nyanja ya teknolojia.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inaidhinisha karibu dola bilioni 190 (euro bilioni 156) za uwekezaji unaolenga kuimarisha utafiti na teknolojia ya Marekani.

Muswada huo unatarajiwa kupitishwa na Baraza la Wawakilishi kabla ya kupelekwa Ikulu kwa Rais wa Marekani Joe Biden kutia saini.

Joe Biden amekaribisha muswada huo: "Tuko kwenye mashindano ya kushinda karne ya 21, na idhni tayari imetolewa .... Hatuwezi kuchukuwa hatari ya kuchelewa."

Kiongozi wa wengi kutoka chama cha Dmocratic katika Bunge la  Seneti Chuck Schumer, ameonya juu ya athari mbaya za kutokuwa na ufadhili wa utafiti kushindana na China.

"Ikiwa hatufanyi chochote, siku zetu kama nchi yenye nguvu kubwa duniani zinaweza kufikia tamati. Hatuna nia ya kuziacha siku hizo zituishiane mbele ya macho yetu," amesema.