MAREKANI-UHAMIAJI

Marekani na Mexico zafungua "ukurasa mpya" katika uhusiano

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador katika Jiji la Mexico Juni 8, 2021.
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador katika Jiji la Mexico Juni 8, 2021. REUTERS - CARLOS BARRIA

Marekani na Mexico zimeanzisha enzi mpya katika uhusiano wao ambao awali ulikuwa umeingiliwa na dosari baada ya utawala wa Donald Trump kuchukuwa hatua ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini Marekani na kuanzisha ujenzi wa ukuta kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Jumanne wiki hii Rais wa Mexico alimpokea makamu wa rais wa Amerika huko Mexico mwishoni mwa ziara yake ya kwanza ya kimataifa ambayo ilimpeleka nchini Guatemala. Nchi hizo mbili zimekubali kushughulikia suala la wahamiaji kupitia ushirikiano na usaidizi kwa nchi za Amerika ya Kati.

Wahamiaji waliowasili, hasa kutoka Honduras, Guatemala na El Salvador, walifikia kiwango cha juu zaidi katika miaka 15 mnamo mwezi wa Aprili, na karibu watu 180,000 walikamatwa mpakani.

Makamu wa rais wa Marekani alimaliza, Jumanne, Juni 8, ziara yake ya kwanza ya kimataifa tangu aingie madarakani mwezi Januari. Ziara hii ya siku mbili, ililenga maswala ya uhamiaji, ambayo ilimpeleka kwanza Guatemala na kisha nchini Mexico. Rais Andrés Manuel López Obrador (AMLO) alimpokea kwa mazungumzo marefu huko Mexico kujadili maswala mbalimbali kati ya nchi hizo mbili.

Itifaki ya makubaliano

"Enzi mpya" inaanza katika uhusiano kati ya Marekani na Mexico, alisema Kamala Harris, ambaye alisifu "majadiliano ya ukweli" na rais wa Mexico. Kwa kuongezea, nchi hizo mbili zimeonyesha kuwa matatizo yao ya pamoja yanayohusiana na wahamiaji: wamesaini hati ya makubaliano ya kushughulikia sababu kuu za uhamiaji katika nchi wahamiaji wanakotoka.

Hapa ndipo ndipo watu wanapaswa kufikiria, kulingana na Rais López Obrador. "Hakuna mtu anayehama, akiacha familia yake, kwa hiari. Watu wanaondoka kwa sababu mbalimbali tena muhimu, amesema. Suluhisho sio kuchukuwa hatua kali. Tunapaswa kutoa njia mbadala. Na bora itakuwa ikiwa watu hawa wangeweza kufanya kazi na kukumbuka nchi wanakotoka. "

"Ni muhimu kuweka kipaumbele kwa kile kinachotokea mpakani na lazima tutoe kipaumbele" kwa sababu ambazo zinasababisha maelfu ya watu wanaondoka katika nchi zao na kukimbilia Marekani, alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano na rais wa Mexico. Bi Harris pia alisema atakwenda mpakani mwenyewe kujionea hali ya mambo kwa tarehe ambayo hakuitaja.