MAREKANI-USHIRIKIANO

"America is back" : Joe Biden aanza ziara yake ya kwanza ya kigeni

Rais wa Marekani Joe Biden, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Cornwall, Uingereza, Jumatano Juni 9, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Cornwall, Uingereza, Jumatano Juni 9, 2021. © REUTERS - PHIL NOBLE

Rais wa Marekani ameondoka Washington kwa ziara yake ya kwanza ya kigeni. Ameanzia ziara yake hiyo nchini Uingereza, ambapo aliwasili Jumatano jioni kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson na kushiriki mkutano wa kilele wa kundi la mataifa 7 yaliyostawi zaidi kiuchumi duniani, G7.

Matangazo ya kibiashara

Joe Biden atakwenda pia Brussels na Geneva ambapo atakutana na Vladimir Poutine. Rais wa Marekani anatarajia kunufaika na ziara hii ya Ulaya kuwahakikishia washirika wake wa bara hilo juu ya kujitolea kwa Marekani kwa upande wao.

"America is back ", Marekani imerudi, Joe Biden amerejelea mara kadhaa maneneo hayo Jumatano usiku wakati akishuka kwenye ndege yake ya Air Force One  mbele ya wanajeshi wa Marekani kwenye kambi ya kikosi cha wanaanga mashariki mwa Uingereza. "Katika kila hatua ya ziara hii tutaweka wazi kuwa: Marekani imerudi na demokrasia dunia nzima zimeungana kukabiliana na changamoto kubwa na shida muhimu kwa siku zetu za usoni," amesema Joe Biden.

Rais Joe Biden amesifia kujitolea kwa Marekani katika jumuiya ya kujihami ya NATO na kutuma onyo kali kwa Urusi wakati akiwa Uingereza.

Akiwahutubia karibu wanajeshi 1,000 na familia zao katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Uingereza, Biden amesema atawasilisha ujumbe wa wazi kwa Rais wa Urusi Vladmir Putin watapokutana wiki ijayo baada ya kuhudhuria mikutano tofauti ya kilele na NATO na G7 na viongozi wa UIaya.

Biden amesema amedhamiria kuyajenga upya mahusiano ya Marekani na Ulaya na kurekebisha mahusiano na Urusi baada ya miaka minne migumu chini ya Rais Mrepublican Donald Trump, ambaye maamuzi yake ya kuongeza ushuru kwa bidhaa na kujiondoa kwenye mikataba yaliharibu mahusiano na washirika wakuu. Biden atakuwa Uingereza hadi Jumapili.