CUBA-SIASA

Biden aitaka serikali ya Cuba "kusikilza raia wake"

Waandamanaji wenye hasira wanaendelea kuandaman kupinga utawala wa udikteta Cuba, katikati mwa janga la Corona, Havana, Cuba Julai 11, 2021.
Waandamanaji wenye hasira wanaendelea kuandaman kupinga utawala wa udikteta Cuba, katikati mwa janga la Corona, Havana, Cuba Julai 11, 2021. REUTERS - ALEXANDRE MENEGHINI

Rais wa Marekani Joe Biden "ametoa wito kwa utawala wa Cuba kuwasikiliza raai wake na kukidhi mahitaji yao," katika taarifa iliyotolewa Jumatatu na Ikulu ya White House.

Matangazo ya kibiashara

"Tuko pamoja na raia wa Cuba na wito wao mahiri wa kutaka uhuru," amesema Joe Biden katika taarifa hii, kufuatia maandamano ya kihistoria nchini Cuba dhidi ya serikali hiyoJumapili Julai 11.

Awali Washington ilionya Cuba dhidi ya matumizi yoyote ya nguvu yanachochea ghasia dhidi ya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika kote nchini humo jana Jumapili dhidi ya "udikteta".

"Marekani inaunga mkono uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuandamana nchini Cuba, na inalaani vikali matumizi yoyote yenye lengo la kuchochea ghasia au yanayolenga kuhatarisha maisha ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani kama haki yao kwa kudhiirisha hasira zao," Mshauri wa Usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumapili Julai 11, Cuba ilishuhudia tukio la kihistoria. Maandamano ambayo hayajawahi kutokea yalishuhudiwa nchi nzima. Kutoka Mashariki hadi Magharibi, Wacuba walionyesha hasira zao wakiandamana, huku wakiomba "uhuru" na kulaani "utawala wa kiimla". Maandamano yamekuwa yakipigwa marufuku katika kisiwa hicho, kinachotawaliwa na Chama pekee cha Kikomunisti kwa miongo kadhaa.