HAITI

Haiti: Afisa wa zamani wa shirika la Marekani akamatwa baada ya mauaji ya rais

Umati wa watu ulikusanyika karibu na gari lililobeba watu wanaoshukiwa kuwa katika kundi lililomuua rais Jovenel Moïse.
Umati wa watu ulikusanyika karibu na gari lililobeba watu wanaoshukiwa kuwa katika kundi lililomuua rais Jovenel Moïse. © VALERIE BAERISWYL/AFP

Mmoja wa Wamarekani wenye asili ya Haiti waliokamatwa nchini Haiti kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya rais Jovenel Moïse wiki iliyopita alikuwa afisa wa shirika la Marekani la kupambana na biashara ya dawa za kulevya, DEA (Drug Enforcement Administration), mkuu wa shirika hilo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Haiti, wiki iliyopita, iliwakamata Wamarekani wawili wenye asili ya Haiti, Joseph Vincent na James Solages, wanaotuhumiwa kushiriki na raia 26 wa Colombia katika operesheni mbaya dhidi ya rais wa Haiti.

Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina, mwakilishi huyo wa DEA alikataa kusema ni yupi kati ya watu hao wawili alikuwa afisa wa shirika hilo la Marekani.

Katika barua pepe, amebaini kwamba mtuhumiwa aliwasiliana na DEA baada ya kuuawa kwa Jovenel Moïse. Shirika hilo lilimshauri mshukiwa huyo ajisalimishe kwa mamlaka ya Haiti, ameongeza mkuu wa shirika la DEA.

Alisisitiza pia kuwa "watu hawa hawakuchukua hatua kwa niaba ya DEA".

Kulingana na chanzo cha usalama, mtuhumiwa hakuwa tena na nafasi yoyote katika shirika hilo, wakati wa mauaji ya Jovenel Moïse.