MAREKANI-HAKI

Marekani yawafungulia mashitaka raia 4 wa Iran kwa kula njama ya utekaji nyara

Masih Alinejad ni mwandishi wa habari katika Idhaa ya Kiajemi ya Sauti ya Amerika (VOA) - - Persian News Network, ambapo anaandika juu ya maswala ya haki za binadamu nchini Iran.
Masih Alinejad ni mwandishi wa habari katika Idhaa ya Kiajemi ya Sauti ya Amerika (VOA) - - Persian News Network, ambapo anaandika juu ya maswala ya haki za binadamu nchini Iran. REUTERS - LISI NIESNER

Raia wanne wa Iran, wanaoshukiwa kuwa maafisa wa idara ya ujasusi wa Iran, wameshtakiwa kwa kula njama ya kumteka nyara mwandishi wa habari wa Marekani, Wizara ya Sheria ya Marekani imesema katika taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Shtaka lililotolewa Jumanne halikutaja mwanahabari aliyetekwa nyara, lakini shirika al habari la REUTERS limeweza kuthibitisha kuwa mtu uyo ni mwandishi wa habari wa Marekani mwenye alisili ya Iran, Masih Alinejad.

Masih Alinejad ni mwandishi wa habari katika Idhaa ya Kiajemi ya Sauti ya Amerika (VOA) - - Persian News Network, ambapo anaandika juu ya maswala ya haki za binadamu nchini Iran.

Wizara ya Sheria ya Marekani haijajieleza kuhusu mwandishi wa habari aliyelengwa na njama hiyo.

Washukiwa hao wanne "walipanga kumteka nyara na kumpeleka kwa nguvu nchini Iran mwandishi huyo wa habari, ambapo hatma yake ingelikuwa ahatarini," amesema Mwendesha Mashtaka wa Marekani Audrey Strauss.