CUBA

Brazil: Bolsonaro anaweza kufanyiwa upasuaji wa haraka

Daktari wa Jair Bolsonaro aliamua ni bora aende Sao Paulo kwa vipimo zaidi na afanyiwe upasuaji wa dharura wa matatizo ya matumbo.
Daktari wa Jair Bolsonaro aliamua ni bora aende Sao Paulo kwa vipimo zaidi na afanyiwe upasuaji wa dharura wa matatizo ya matumbo. via REUTERS - INSTAGRAM @jairmessiasbolsonaro

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro yuko Sao Paulotanu Jumatano kwa uchunguzi wa kitabibu kufuatia matatizo ya matumbo na anaweza kufanyiwa upasuaji wa dharura, wasaidizi wa kiongozi huyo wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Haya ndiyo matatizo ya mwisho ya kiafya kwa rais huyu, ambaye alichomwa kisu na kufanyiwa upasuaji mara kadhaa muda mfupi kabla ya ushindi wake wa uchaguzi mwaka wa 2018.

Tangazohilikutok ikulu ya rais linakuja wakati umaarufu wa Jair Bolsonaro umepungua katika kura za hivi karibuni juu ya jinsi anavyoshughulikia mgogoro wa kafya unaosababishwa na virusi vya Corona na kashfa ya ufisadi katika serikali yake kuhusiana na ununuzi wa chanjo dhidi ya COVID-19.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jair Bolsonaro mwenye umri wa miaka 66 alituma picha yake, akitabasamu, akiwa amelala kitandani hospitalini kwa uchunguzi.

Hapo awali, kiongozi huyo alikuwa amekwenda katika hospitali ya kijeshi huko Brasilia kwa kile wasaidizi wake walielezea kama alikwenda kufanya vipimo kufuatia kwikwi sugu.

Lakini baadaye, daktari wa Jair Bolsonaro aliamua ni bora aende Sao Paulo kwa vipimo zaidi na afanyiwe upasuaji wa dharura wa matatizo ya matumbo.