CUBA

Cuba: serikali yaonyesjha ishara ya kwanza baada ya maandamano

Kuwezesha kuingia kwa bidhaa muhimu ilikuwa moja ya madai ya raia wa Cuba, wanaokabiliwa na uhaba mkubwa, uliochochewa na mgogoro wa kiuchumi ambao unaikumba nchi hiyo, ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi tangu miaka 30 iliyopita.
Kuwezesha kuingia kwa bidhaa muhimu ilikuwa moja ya madai ya raia wa Cuba, wanaokabiliwa na uhaba mkubwa, uliochochewa na mgogoro wa kiuchumi ambao unaikumba nchi hiyo, ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi tangu miaka 30 iliyopita. YAMIL LAGE AFP

Serikali ya Cuba imetangaza hatua za kwanza za kutuliza za kupunguza hasira za raia wake, hasa kwa kuruhusu kuingizwa nchini humo chakula na dawa, siku tatu baada ya maandamano ya kihistoria ambayo yametoa mafunzo makubwa.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Cuba imeamua "kuidhinisha kwa mfumo wa kipekee na kwa muda abiria kuingiza chakula na dawa bila ushuru wa forodha", amesema Waziri Mkuu Manuel Marrero kwenye runinga ambapo ameonekana akiandamana na Rais Miguel Diaz-Canel na mawaziri kadhaa.

Kuwezesha kuingia kwa bidhaa muhimu ilikuwa moja ya madai ya raia wa Cuba, wanaokabiliwa na uhaba mkubwa, uliochochewa na mgogoro wa kiuchumi ambao unaikumba nchi hiyo, ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi tangu miaka 30 iliyopita.

Katika barua ya wazi iliyochapishwa hivi karibuni, kundi la wasanii na wasomi walikuwa wanaomba hatua kama hiyo.

Waziri wa Uchumi Alejandro Gil, kwa upande wake, ametangaza kumalizika kwa kikomo cha mishahara katika makampuni na mashirika yanayomilikiwa na serikali, ambayo yalikuwa chini ya kiwango kikubwa cha mishahara.

"Tunaondoa kikomo kwenye kiwango cha mshahara kwa makampuni yanayomilikiwa na serikali, kama hatua ya kwanza", kulingana na "kanuni ya kupata zaidi ikiwa tunazalisha utajiri zaidi na ikiwa tuna ufanisi zaidi".

Hatimaye, Waziri Mkuu amesema kuwa raia wanaweza kuhamia mji mwingine kwa muda na kunufaika na kitabu cha ugavi, wakati ilikuwa haiwezekani hapo awali.

- "Wito wa amani" -

Hatua hizi zinatangazwa siku tatu baada ya maandamano Jumapili wakati maelfu ya Wacuba walipoingia barabarani katika miji na vijiji zaidi ya 40 wakipiga kelele "Tuna njaa", "Tunataka Uhuru" na "Tunapinga  udikteta".