HAITI-USALAMA

Colombia yamtaja mshukiwa mkuu wa mauaji ya Jovenel Moïse

Mkuu wa Polisi wa Haiti Léon Charles azungumza katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mauaji ya rais Jovenel Moise, huko Port-au-Prince, Haiti, Julai 11, 2021.
Mkuu wa Polisi wa Haiti Léon Charles azungumza katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mauaji ya rais Jovenel Moise, huko Port-au-Prince, Haiti, Julai 11, 2021. AFP - VALERIE BAERISWYL

Afisa wa zamani wa wizara ya Sheria ya Haiti, Joseph Felix Badio, anaweza kuwa aliamuru mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moïse, mkuu wa polisi wa Colombia Jenerali Jorge Vargas amesema.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa Haiti aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 7 na kundi la watu katika makazi yake karibu na mji wa Port-au-Prince. Kundi hili lilikuwa na Wacolombia 26 na Wamarekani 2 wenye asili ya Haiti, kulingana na mamlaka huko Port-au-Prince.

Ushahidi wa kwanza wa uchunguzi unaonyesha kwamba Joseph Felix Badio alitoa agizo la kumuua Jovenel Moïse siku tatu kabla ya shambulio hilo, amesema Jenerali Jorge Vargas katika ujumbe uliorekodiwa.

"Siku kadhaa kabla, Joseph Felix Badio, ambaye alikuwa afisa wa zamani wa Wizara ya Sheria (Haiti), ambaye alikuwa anafanya kazi katika kitengo cha kupambana na ufisadi katika idara ya ujasusi, aliwaambia wanajeshi wa zamani wa Colombia Duberney Capador na German Rivera kwamba wanatakiwa kumuua rais wa Haiti, "amesema.

Duberney Capador na German Rivera hapo awali walitafutwa kwa ajili ya kutoa ulinzi.

Polisi wa Colombia wanashirikiana na mamlaka ya Haiti kuwahoji raia 18 wa Colombia waliokamatwa tangu kuuawa ka raid Moise. Wengine watano bado wako mafichoni na watatu waliuawa, ikiwa ni pamoja na Capador.