MAREKANI

Washington yamuwekea vikwazo waziri wa ulinzi wa Cuba kuhusiana na maandamano

Marekani, imesisitiza, "sheria kamili iliyopitishwa chini ya utawala Obama, inapaswa kutumika, sheria ambayo inaruhusu kuanzishwa kwa vikwazo ikiwa kuna ukiukaji wa haki za binadamu, kwa vitendo vya kila siku vya ukandamizaji na vurugu za polisi ambazo ziligharimu maisha ya watu 1,201 mwaka 2020 ” nchini Cuba.
Marekani, imesisitiza, "sheria kamili iliyopitishwa chini ya utawala Obama, inapaswa kutumika, sheria ambayo inaruhusu kuanzishwa kwa vikwazo ikiwa kuna ukiukaji wa haki za binadamu, kwa vitendo vya kila siku vya ukandamizaji na vurugu za polisi ambazo ziligharimu maisha ya watu 1,201 mwaka 2020 ” nchini Cuba. ADALBERTO ROQUE AFP

Marekani imetangaza kuchukuwa vikwazo vya kifedha dhidi ya Waziri wa Ulinzi wa Cuba Alvaro Lopez Miera na kitengo maalum cha Wizara ya Mambo ya Ndani, kilichohusika kulingana na rais wa Marekani kwa "ukandamizaji" wa hivi karibuni "dhidi ya maandamano ya amani" , yanayounga mkono demokrasia ”nchini Cuba.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi vipya "ni mwanzo tu," ameonya Joe Biden. Na kuongeza: "Marekani itaendelea kuwachukulia vikwazo wale wanaohusika na ukandamizaji dhidi ya raia wa Cuba. Rais wa Marekani ameahidi kuendelea kushinikiza kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa. Hatua zilizoelezwa kwenye mtandao wa Twitter na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, kama "zisizo na msingi na za kibaguzi"

Marekani, imesisitiza, "sheria kamili iliyopitishwa chini ya utawala Obama, inapaswa kutumika, sheria ambayo inaruhusu kuanzishwa kwa vikwazo ikiwa kuna ukiukaji wa haki za binadamu, kwa vitendo vya kila siku vya ukandamizaji na vurugu za polisi ambazo ziligharimu maisha ya watu 1,201 mwaka 2020 ” nchini Cuba.

Joe Biden amekosolewa na Warepublican na jamii ya Wacuba huko Florida kwa kushindwa kuonyesha mara moja uungwaji wake mkono kwa kile kinachoonekana kama maandamano makubwa zaidi ya serikali katika miongo kadhaa. Lakini pia yuko chini ya shinikizo kutoka upande wa mrengo wa kushoto wa Chama cha Democratic, ambacho kinataka kukomeshwa kwa vikwazo vilivyowekwa chini ya utawala wa Donald Trump.