VENEZUELA-SIASA

Venezuela: Maduro kujadili na upinzani mwezi wa Agosti

Nicolas Maduro amesema anataka vikwazo vya Marekani ambavyo viliathiri sekta ya fedha na mafuta viondolewe.
Nicolas Maduro amesema anataka vikwazo vya Marekani ambavyo viliathiri sekta ya fedha na mafuta viondolewe. Handout Venezuelan Presidency/AFP

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema yuko tayari kusafiri kwenda Mexico kuanza mazungumzo na upinzani mwezi ujao kama sehemu ya upatanishi ulioanzishwa na Norway, mchakato ambao anatarajia kuona Marekani ikishiriki

Matangazo ya kibiashara

Upinzani nchini Venezuela ulibadilisha mkakati wake mwezi wa Mei kwa kutangaza nia yake ya kuanza tena mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa kisiasa unaoathiri nchi hiyo.

Venezuela, mwanachama wa OPEC, imekuwa akikabiliwa na mzozo tangu kuchaguliwa tena kwa Nicolas Maduro kuwa rais mwaka 2018, uchaguzi ambao ulipingwa na upinzani. Wapinzani wake, pamoja na Marekani na Umoja wa Ulaya, pia wanamshutumu kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu, madai ambayo anakanusha.

Wanadiplomasia wakuu huko Washington, Brussels na Ottowa, hata hivyo, mwezi Juni walisema wako tayari kupitia vizuizi vilivyowekwa kwa serikali ya Nicolas Maduro ikiwa mazungumzo na wapinzani hayatozaa matunda yoyotea, hali ambao inapania kufungua njia ya uchaguzi mpya huru na wa haki.

"Ninaweza kuwaambia kuwa tuko tayari kwenda Mexico," amesema Nicolas Maduro katika mahojiano na kituo cha runinga cha serikali cha Telesur na kurushwa Jumamosi jioni. "Tulianza kujadili mpango mgumu na wenye usumbufu," ameongeza.

Juan Guaido aungwa mkono na nchi kadhaa za Amerika

Utawala wa Joe Biden na nchi zingine zinamtambua kiongozi wa upinzaji wa Venezuela Juan Guaido kama rais halali wa Venezuela.

Nicolas Maduro amesema anataka vikwazo vya Marekani ambavyo viliathiri sekta ya fedha na mafuta viondolewe.