MAREKANI

Biden ashutumu Urusi kwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa wabunge wa 2022

Rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya maafisa wa Idara ya ujasusi huko McLean, Virginia, Julai 27, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya maafisa wa Idara ya ujasusi huko McLean, Virginia, Julai 27, 2021. AP - Susan Walsh

Rais wa Marekani Joe Biden ameikosoa Urusi kwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani uliopangwa kufanyika 2022 kwa kueneza "habari mbaya". Taarifa iliyotangulia mkutano Jumatano hii, Julai 28 kati ya Manaibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na Marekani, zaidi ya mwezi mmoja baada ya mkutano wa Geneva kati ya Joe Biden na Vladimir Putin.

Matangazo ya kibiashara

"Angalia kile Urusi imefanya kuhusiana na uchaguzi wa 2022 na habari mbaya. Ni ukiukaji dhahiri wa uhuru wa nchi yetu! Joe Biden hakutaka kupitisha upande maneno yake wakati alipozuru Ofisi ya kitaifa idara ya Upelelezi karibu na mji wa Washington, akimaanisha habari anayopokea juu ya suala hili wakati wa mkutano wa kila siku.

Katika msimu wa 2022, kutafanyika uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani, ambapo viti vyote katika Baraza la Wawakilishi na theluthi moja ya viti katika Bunge la Seneti vinapitiwa upya.

Rais wa Marekani pia alimshambulia mwenzake wa Urusi Vladimir Poutine: rais wa Urusi "ana tatizo kweli keli, yeye ndiye kiongozi wa nchi yenye uchumi ambayo ina silaha za nyuklia na visima vya mafuta na sio kitu kingine chochote. Hiyo inamfanya awe hatari zaidi kwa maoni yangu. "