MAREKANI-AFYA

Marekani kutoa dola 100 kwa kila atakayepigwa chanjo ya COVID-19

Rais wa Marekani Joe Biden azungumzia juu ya chanjo ya Covid-19 katika ikulu ya White House.
Rais wa Marekani Joe Biden azungumzia juu ya chanjo ya Covid-19 katika ikulu ya White House. SAUL LOEB AFP

Rais wa Marekani Joe Biden, amezitaka serikali za mitaa nchini humo kuanza kuwalipa watu fedha ili wachome chanjo za kuzuia maambukizi ya Covid 19.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, ametaka watu ambao hawajapata chanjo kuvaa barakoa kila wakati wakiwa kwenye maeneo yenye watu na kupimwa maambukizi hayo.

Hatua hii imekuja kufuatia ongezeko la maambukizi yanayosababishwa na kirusi Delta, ambacho kinasambaa kwa kasi hasa kwa watu ambao hawajapokea chanjo.

Marekani inashika mkia miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa viwango vya watu waliochanjwa, licha ya kuwa na chanjo za kutosha zinazotolewa bure.

Juhudi za Ikulu ya Marekaniza kuhamasisha wananchi kuchanjwa zimegonga ukuta, hasa kutokana na vuguvugu kubwa linalopinga chanjo hiyo, habari za uwongo zinazosambazwa kuhusu chanjo pamoja na migawanyiko ya kisiasa.