MAREKANI-USALAMA

Afisa wa polisi auawa katika urushianaji risasi karibu na Pentagon

Maafisa wa vikosi vya usalama karibu na mlango wa Pentagon baada ya mauaji ya afisa wa polisi.
Maafisa wa vikosi vya usalama karibu na mlango wa Pentagon baada ya mauaji ya afisa wa polisi. Olivier DOULIERY AFP

Afisa wa polisi anayelinda Pentagon, makao makuu ya jeshi nchini Marekani aliuawa Jumanne nje ya jengo hilo, lililoko Arlington, Virginia, Seneta wa Marekani Mark Warner amesema.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu idara inayohusika na ulinzi wa makao makuu ya Idara ya Ulinzi na Usalama wa jeshi nchini Marekani amesema kuwa ufyatulianaji risasi katika kituo cha basi kilicho karibu na Pentagon umesababisha majeraha kadhaa.

Woodrow Kuss alikataa kusema ikiwa ikiwa tukio hilo limesababisha vifo vyovyote na hakutaka uelezea sababu za tukio hilo.

FBI inashirikiana na idara zingine kwa uchunguzi, ameongeza, bila kubainisha ikiwa mshukiwa amekamatwa, lakini akibaini kwamba hakuna operesheni ya polisi iliyofanyika.

Pentagon ilizingirwa kwa saa kadhaa baada ya tukio hilo.