MAREKANI

Marekani yataka wahamiaji kuchanjwa

Wahamiaji wa Cuba huko Ciudad Juarez kwenye mpaka wa Mexico. Walipowasili kwa ndege kutoka Panama, wanaenda Marekani.
Wahamiaji wa Cuba huko Ciudad Juarez kwenye mpaka wa Mexico. Walipowasili kwa ndege kutoka Panama, wanaenda Marekani. REUTERS/Jose Luis Gonzalez

Utawala wa Joe Biden unajiandaa kupendekeza wahamiaji walio chini ya ulinzi wa nchi hiyo katika mpaka wa Mexico kupewa chanjo dhidi ya COVID-19, Gazeti la Washington Post limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na utaratibu wa mpango huu mpya, Wizara ya Usalama wa Ndani itatoa chanjo kwa wahamiaji muda mfupi baada ya kuingia nchini Marekani, gazeti hilo limesema, likinukuu maafisa wawili wa wizara hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao.

Kufikia sasa, ni idadi ndogo tu ya wahamiaji ambao wamepewa chanjo wakati wako katika vituo vya idara ya Uhamiaji na Forodha wa Merika, Washington Post ilisema.

Mpango huo bado haujakamilika, Gazeti la Washington Post limesema.