MAREKANI

Marekani kuendeleza mpango unaowataka wasafiri wa kigeni kuchanjwa

Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya janga hilo vimeongezeka nchini Marekani.
Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya janga hilo vimeongezeka nchini Marekani. Karen Ducey GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP

Utawala wa Biden unaendeleza mpango wa kuwataka wasafiri wa kigeni wanaoingia Marekani kupewa chanjo kamili dhidi ya Covid-19, amesema mmoja wa maafisa wa ikulu ya White kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Matangazo ya kibiashara

White House inataka kufunguliwa usafiri bila hata hivyo kuondoa vizuizi hidi ya Corona, na idadi ya visa vipya vya maambukizi ya janga hilo vimeongezeka nchini Marekani.

Makundi mbalimbali ya wataalam yanaendelea "mfumo mpya ambao utatekelezwa wakati tukuwa tufungua mipaka," ameongeza afisa huyo.

Mfumo huu ni pamoja na "mbinu ya kuendelea ambayo, baada ya muda, itaonyesha, kwa tofauti ndogo, kwamba raia wa kigeni wanaosafiri nchini Marekani watalazimika kupewa chanjo kamili."

Hoja hii ni ishara tosha kwa wakati huu ambapo White House Nimekuwa ikijianda kuondoa vikwazo dhidi ya Corona.