MAREKANI

Mpango wa kufufua uchumi wa Biden wazuiwa na seneta wa Democratic

Mpango wa mageuzi wa Biden wasitishwa kwa kura ya Seneta wa chama cha Democratic Joe Manchin.
Mpango wa mageuzi wa Biden wasitishwa kwa kura ya Seneta wa chama cha Democratic Joe Manchin. ALEX WONG GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP

Seneta wa Jimbo la West Virginia kutoka chama cha Democratic Joe Manchin amesema kuwa hataunga mkono dola trilioni 3.5 katika uwekezaji ambao rais wa Marekani Joe Biden anataka.

Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanza kwa majadiliano juu ya mpango huu wa mageuzi, Joe Manchin amekuwa kiungo dhaifu zaidi katika kambi ya Democratic. Mara kadhaa, ameelezea mashaka, na hivyo kuwa seneta mwenye kutaka ushawishi na hata kujifaharisha ili kupata kura katika Bunge la Seneti. Lakini wakati Maseneta wa chama cha Democratic wakifikiria kuwa wana uungwaji mkono wa maseneta wote kwa tiketi ya chama hicho, seneta kutoka West Virginia ameamua kuonyesha msimamo wake na kuzuia mpango huo.

Hii inaweza kutatiza kazi ya Chuck Schumer, kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti. "Hatapata kura yangu na Chuck anafahamu hilo. Tayari tumezungumza juu hilo. Tayari tumetoa dola bilioni 5,000 kufufua uchumi na kuwasaidia Wamarekani kadiri tuwezavyo. "

Mpango wa Joe Biden, nguzo muhimu ya sera yake ya Build Back Better, "kuijenga upya Marekani" utagharimu zaidi ya dola Trilioni 3 kwa miaka 10 ijayo kwa mageuzi ya kina kwa shule, hospitali, makaazi ya kuishi na Tabia nchi.

Chama cha Democratic kinahitaji kura za maseneta wote waliochaguliwa kwa tiketi ya chama hicho ili kuweza kupitisha mpango huo wa Joe Biden. Kwa hivyo hawawezi kupoteza kura ya Joe Manchin ambaye anasema itabidi apate ushawishi wa kutosha ili aweze kubadili msimamo wake.

Siku ya Jumapili Seneta huyo alisema kwamba lazima wachukue muda wa kutosha wa kujadili suala hilo na wasiharakie. Wakati Ikulu ya White House ilitarajia mpango huo kupigiwa kura haraka iwezekanavyo