MAREKANI-SIASA

Biden ziarani California kumuunga mkono gavana anayetishiwa kufutwa kazi

Joe Biden alikuja kumuunga mkono Gavana wa chama cha Democratic Gavin Newsom mnamo Septemba 12, 2021 huko Long Beach, California.
Joe Biden alikuja kumuunga mkono Gavana wa chama cha Democratic Gavin Newsom mnamo Septemba 12, 2021 huko Long Beach, California. Getty Images via AFP - DAVID MCNEW

Rais wa Marekani alikuwa ziarani katika jimbo la California Jumatatu, Septemba 13, kumuunga mkono Gavana wa Jimbo la hilo kutoka chama cha Demmocratic Gavin Newsom. 

Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii, Septemba 14, wakaazi wa California wanapiga kura kuamua ikiwa wamuondoe mamlakani au la. Kutokana na hali hii, Joe Biden ujifikia mwenyewe katika jimbo la California ili kuonyesha mshikamano wake na Gavana Gavin Newsom.

Hakuongea kwa muda mrefu, lakini aliongea wazi. Bila kutaja jina la Larry Elder, Joe Biden alinyesha picha ya mpinzani mkuu wa Gavin Newsom.

"Gavana wa chama cha Republican anayezuia maendeleo dhidi ya janga la Covid-19, ambaye pia ni haungi mkono maendeleo ya wanawake na ambaye anapinga wafanyikazi, ambaye haamini uchaguzi wa huru," alisema rais wa Marekani. Chaguo, linapaswa kuwa wazi kabisa: Gavin Newsom. Pamoja na Gavin, mna gavana atakaye wahakikishia kuwa siasa za giza, mbovu, na za uharibifu za Donald Trump hazipati nafasi hapa California. "

Kuiangusha kambi ya Trump

Mgombea mkuu wa chama cha Republican anaunga mkono hoja za Donald Trump, hasa kuhusu udanganyifu katika uchaguzi wa urais uliyopita. Na kwa upande wa Gavin Newsom, anapinga hoja hiyo.

"Labda tulimuangusha Donald Trump, lakini hatukuziangusha nguzo zake," Gavin Newsom alionya. Nguzo zake ziko kwenye kadi za kupiia kura hapa California. Na ndio sababu ni muhimu sana. Sio kwetu tu, watu milioni 40 wa jimbo kubwa na lenye watu wengi, lakini pia kutuma ujumbe kwa Marekani yote. "

Kura za hivi karibuni ni nzuri kwa Gavin Newsom. Lakini mnamo 2003, ilikuwa kupitia utaratibu huo wa raia kutokuwa na imani na gavana wa California ambapo Arnold Schwarzenegger alikuwa gavana wa mwisho wa chama cha Republican wa California.